Marko 15:17
Mark 15:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani.
Mark 15:17 in English
Mark 15:17 · Berean Standard Bible
They dressed Him in a purple robe, twisted together a crown of thorns, and set it on His head.
Context
15Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe. 16Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio,* wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17Wakamvalisha Yesu joho la zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani. 18Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 19Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.