Native Bible

Mark 15:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!”

Mark 15:14 in English

Mark 15:14 · Berean Standard Bible

“Why?” asked Pilate. “What evil has He done?” But they shouted all the louder, “Crucify Him!”

Context

12Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?” 13Wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe!” 14Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!” 15Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe. 16Askari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio,* wakakusanya kikosi kizima cha askari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.