Marko 14:60
Mark 14:60 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?”
Mark 14:60 in English
Mark 14:60 · Berean Standard Bible
So the high priest stood up before them and questioned Jesus, “Have You no answer? What are these men testifying against You?”
Context
58“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana. 60Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 61Lakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote.
Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo,* Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?” 62Yesu akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.