Native Bible

Mark 10:44 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote.

Mark 10:44 in English

Mark 10:44 · Berean Standard Bible

and whoever wants to be first must be the slave of all.

Context

42Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 43Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 44na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote. 45Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.” 46Kisha wakafika Yeriko. Yesu alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.