Marko 10:37
Mark 10:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamwambia, “Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.”
Mark 10:37 in English
Mark 10:37 · Berean Standard Bible
They answered, “Grant that one of us may sit at Your right hand and the other at Your left in Your glory.”
Context
35Kisha Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie lolote tutakalokuomba.” 36Naye akawaambia, “Je, mwataka niwafanyie jambo gani?” 37Wakamwambia, “Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.” 38Lakini Yesu akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?” 39Wakajibu, “Tunaweza.”
Kisha Yesu akawaambia, “Kikombe nikinyweacho mtakinywea na ubatizo nibatizwao mtabatizwa,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.