Native Bible

Mark 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.’ ”

Mark 1:3 in English

Mark 1:3 · Berean Standard Bible

“A voice of one calling in the wilderness, ‘Prepare the way for the Lord, make straight paths for Him.’”*

Context

1Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako”: 3“sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.’ ” 4Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 5Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.