Marko 1:15
Mark 1:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.”
Mark 1:15 in English
Mark 1:15 · Berean Standard Bible
“The time is fulfilled,” He said, “and the kingdom of God is near. Repent and believe in the gospel!”
Context
13naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia. 14Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, 15akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.” 16Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 17Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.