Native Bible

Micah 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia.

Micah 1:3 in English

Micah 1:3 · Berean Standard Bible

For behold, the LORD comes forth from His dwelling place; He will come down and tread on the high places of the earth.

Context

1Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu. 2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake, ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu. 3Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia. 4Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko. 5Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.