Mathayo 8:25
Matthew 8:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!”
Matthew 8:25 in English
Matthew 8:25 · Berean Standard Bible
The disciples went and woke Him, saying, “Lord, save us! We are perishing!”
Context
23Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. 24Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!” 26Naye Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa. 27Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.