Mathayo 4:22
Matthew 4:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.
Matthew 4:22 in English
Matthew 4:22 · Berean Standard Bible
and immediately they left the boat and their father and followed Him.
Context
20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 21Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita. 22Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata. 23Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu. 24Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.