Mathayo 4:17
Matthew 4:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”
Matthew 4:17 in English
Matthew 4:17 · Berean Standard Bible
From that time on Jesus began to preach, “Repent, for the kingdom of heaven is near.”
Context
15“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,
kwenye njia ya kuelekea baharini,
ngʼambo ya Yordani,
Galilaya ya watu wa Mataifa: 16watu wale waliokaa gizani
wameona nuru kuu;
nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti,
nuru imewazukia.” 17Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.” 18Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 19Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.