Mathayo 26:49
Matthew 26:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mara Yuda akamjia Yesu na kumsalimu, “Salamu, Rabi!” Akambusu.
Matthew 26:49 in English
Matthew 26:49 · Berean Standard Bible
Going directly to Jesus, he said, “Greetings, Rabbi!” and kissed Him.
Context
47Alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Alikuwa amefuatana na umati mkubwa wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. 48Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.” 49Mara Yuda akamjia Yesu na kumsalimu, “Salamu, Rabi!” Akambusu. 50Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.”
Kisha wale watu wakasogea mbele, wakamkamata Yesu. 51Ghafula mmoja wa wale waliokuwa na Yesu alipoona hivyo, akaushika upanga wake, akauchomoa na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.