Mathayo 26:15
Matthew 26:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha.
Matthew 26:15 in English
Matthew 26:15 · Berean Standard Bible
and asked, “What are you willing to give me if I hand Him over to you?” And they set out for him thirty pieces of silver.
Context
13Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.” 14Kisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 15na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu. 17Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.