Mathayo 25:19
Matthew 25:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao.
Matthew 25:19 in English
Matthew 25:19 · Berean Standard Bible
After a long time the master of those servants returned to settle accounts with them.
Context
17Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi. 18Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alikwenda akachimba shimo ardhini na kuificha ile fedha ya bwana wake. 19“Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao. 20Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta nyingine tano zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta tano zaidi.’ 21“Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.