Mathayo 24:7
Matthew 24:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali.
Matthew 24:7 in English
Matthew 24:7 · Berean Standard Bible
Nation will rise against nation, and kingdom against kingdom. There will be famines and earthquakes in various places.
Context
5Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’* nao watawadanganya wengi. 6Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu. 9“Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.