Mathayo 24:45
Matthew 24:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?
Matthew 24:45 in English
Matthew 24:45 · Berean Standard Bible
Who then is the faithful and wise servant, whom the master has put in charge of his household, to give the others their food at the proper time?
Context
43Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. 44Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia. 45“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 46Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 47Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.