Mathayo 21:29
Matthew 21:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Yule mwanawe akamjibu ‘Mimi sitakwenda.’ Baadaye akabadili mawazo yake akaenda.
Matthew 21:29 in English
Matthew 21:29 · Berean Standard Bible
‘I will not,’ he replied. But later he changed his mind and went.*
Context
27Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.”
Naye akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.” 28“Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ 29“Yule mwanawe akamjibu ‘Mimi sitakwenda.’ Baadaye akabadili mawazo yake akaenda. 30“Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda, bwana,’ lakini hakwenda. 31“Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?”
Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.”
Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.