Mathayo 13:34
Matthew 13:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano.
Matthew 13:34 in English
Matthew 13:34 · Berean Standard Bible
Jesus spoke all these things to the crowds in parables. He did not tell them anything without using a parable.
Context
32Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.” 33Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.” 34Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano. 35Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema:
“Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano;
nitahubiri mambo yaliyofichika
tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.” 36Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.