Mathayo 13:28
Matthew 13:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’ “Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayangʼoe?’
Matthew 13:28 in English
Matthew 13:28 · Berean Standard Bible
‘An enemy did this,’ he replied. So the servants asked him, ‘Do you want us to go and pull them up?’
Context
26Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea. 27“Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’ 28“Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’
“Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayangʼoe?’ 29“Lakini akasema, ‘Hapana, msiyangʼoe, kwa maana wakati mkingʼoa magugu mnaweza mkangʼoa na ngano pamoja nayo. 30Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.