Native Bible

Matthew 13:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.

Matthew 13:26 in English

Matthew 13:26 · Berean Standard Bible

When the wheat sprouted and bore grain, then the weeds also appeared.

Context

24Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea. 27“Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’ 28“Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’ “Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayangʼoe?’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.