Native Bible

Matthew 12:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”

Matthew 12:38 in English

Matthew 12:38 · Berean Standard Bible

Then some of the scribes and Pharisees said to Him, “Teacher, we want to see a sign from You.”

Context

36Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena. 37Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” 38Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. 40Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi* kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.