Mathayo 11:12
Matthew 11:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka.
Matthew 11:12 in English
Matthew 11:12 · Berean Standard Bible
From the days of John the Baptist until now, the kingdom of heaven has been subject to violence,* and the violent lay claim to it.
Context
10Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:
“ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako.’ 11Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yohana. 12Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. 13Kwa maana manabii wote na Sheria walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14Ikiwa mko tayari kukubali hilo, yeye ndiye yule Eliya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.