Luka 9:13
Luke 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.”
Luke 9:13 in English
Luke 9:13 · Berean Standard Bible
But Jesus told them, “You give them something to eat.” “We have only five loaves of bread and two fish,” they answered, “unless we go and buy food for all these people.”
Context
11Lakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji. 12Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Yesu na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.” 13Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”
Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.” 14Walikuwako wanaume wapatao 5,000.
Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.” 15Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.