Luka 8:32
Luke 8:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu.
Luke 8:32 in English
Luke 8:32 · Berean Standard Bible
There on the hillside a large herd of pigs was feeding. So the demons begged Jesus to let them enter the pigs, and He gave them permission.
Context
30Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?”
Akamjibu, “Legioni,”* kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno. 31Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo.* 32Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu. 33Wale pepo wachafu walipomtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremkia gengeni kwa kasi, likatumbukia ziwani na kuzama. 34Wale watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe walipoona yaliyotukia, wakakimbia, wakaeneza habari hizi mjini na mashambani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.