Luka 8:31
Luke 8:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo.*
Luke 8:31 in English
Luke 8:31 · Berean Standard Bible
And the demons kept begging Jesus not to order them to go into the Abyss.
Context
29Wakati huo Yesu alikuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke huyo mtu. Mara nyingi huyo pepo mchafu alimpagaa, na hata alipofungwa kwa minyororo mikono na miguu na kuwekwa chini ya ulinzi, alikata hiyo minyororo na kupelekwa na huyo pepo mchafu kwenda nyikani. 30Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?”
Akamjibu, “Legioni,”* kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno. 31Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo.* 32Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu. 33Wale pepo wachafu walipomtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremkia gengeni kwa kasi, likatumbukia ziwani na kuzama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.