Luka 6:5
Luke 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”
Luke 6:5 in English
Luke 6:5 · Berean Standard Bible
Then Jesus declared, “The Son of Man is Lord of the Sabbath.”
Context
3Yesu akawajibu, “Je, ninyi hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa? 4Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.” 5Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” 6Ikawa siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. 7Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.