Native Bible

Luke 24:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia.

Luke 24:14 in English

Luke 24:14 · Berean Standard Bible

They were talking with each other about everything that had happened.

Context

12Hata hivyo, Petro akainuka na kukimbia kwenda kule kaburini. Alipoinama kuchungulia, akaona vile vitambaa vya kitani, ila hakuona kitu kingine. Naye akaenda zake akijiuliza nini kilichotokea. 13Ikawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba* kutoka Yerusalemu. 14Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. 15Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 16lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.