Luka 20:15
Luke 20:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.” “Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa?
Luke 20:15 in English
Luke 20:15 · Berean Standard Bible
So they threw him out of the vineyard and killed him. What then will the owner of the vineyard do to them?
Context
13“Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’ 14“Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ 15Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.”
“Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa? 16Atakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.”
Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!” 17Lakini Yesu akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa:
“ ‘Jiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni’?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.