Luka 2:35
Luke 2:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.”
Luke 2:35 in English
Luke 2:35 · Berean Standard Bible
so that the thoughts of many hearts will be revealed— and a sword will pierce your soul as well.”
Context
33Naye Yosefu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. 34Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, 35ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.” 36Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa. 37Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.