Luka 19:10
Luke 19:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”
Luke 19:10 in English
Luke 19:10 · Berean Standard Bible
For the Son of Man came to seek and to save the lost.”
Context
8Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.” 9Ndipo Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu. 10Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” 11Walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo. 12Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.