Luka 18:23
Luke 18:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Aliposikia jambo hili, alisikitika sana kwa maana alikuwa mtu mwenye mali nyingi.
Luke 18:23 in English
Luke 18:23 · Berean Standard Bible
But when the ruler heard this, he became very sad, because he was extremely wealthy.
Context
21Akajibu, “Amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.” 22Yesu aliposikia haya, akamwambia, “Bado kuna jambo moja ulilopungukiwa. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 23Aliposikia jambo hili, alisikitika sana kwa maana alikuwa mtu mwenye mali nyingi. 24Yesu akamtazama, akasema, “Tazama jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! 25Hakika ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.