Luka 14:29
Luke 14:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki,
Luke 14:29 in English
Luke 14:29 · Berean Standard Bible
Otherwise, if he lays the foundation and is unable to finish the work, everyone who sees it will ridicule him,
Context
27Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? 29La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, 30wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’ 31“Au ni mfalme gani atokaye kwenda kupigana vita na mfalme mwingine, ambaye hakai chini kwanza na kufikiri iwapo akiwa na jeshi la watu 10,000 ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu 20,000?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.