Luka 14:11
Luke 14:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”
Luke 14:11 in English
Luke 14:11 · Berean Standard Bible
For everyone who exalts himself will be humbled, and the one who humbles himself will be exalted.”
Context
9Kama mkifanya hivyo yule aliyewaalika ninyi wawili atakuja na kukuambia, ‘Mpishe huyu mtu kiti chako.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kukaa katika nafasi ya chini kabisa. 10Badala yake, unapoalikwa, chagua nafasi ya chini, ili yule mwenyeji wako atakapokuona atakuja na kukuambia, ‘Rafiki yangu, nenda kwenye nafasi iliyo bora zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wenzako wote. 11Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.” 12Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, wao nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umelipwa kile ulichofanya na kupata thawabu yako. 13Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.