Native Bible

Luke 13:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo.

Luke 13:3 in English

Luke 13:3 · Berean Standard Bible

No, I tell you. But unless you repent, you too will all perish.

Context

1Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Yesu habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. 2Yesu akawauliza, “Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo cha namna hiyo walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 3La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo. 4Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? 5Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.