Native Bible

Luke 12:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa!

Luke 12:49 in English

Luke 12:49 · Berean Standard Bible

I have come to ignite a fire on the earth, and how I wish it were already kindled!

Context

47“Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. 48Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi. 49“Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa! 50Lakini ninao ubatizo ambao lazima nibatizwe, nayo dhiki yangu ni kuu mpaka ubatizo huo ukamilike! 51Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaambia sivyo, nimekuja kuleta mafarakano.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.