Luka 12:44
Luke 12:44 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote.
Luke 12:44 in English
Luke 12:44 · Berean Standard Bible
Truly I tell you, he will put him in charge of all his possessions.
Context
42Yesu akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? 43Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44Amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 45Lakini kama yule mtumishi atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa. 46Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.