Luka 11:16
Luke 11:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wengine ili kumjaribu wakataka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
Luke 11:16 in English
Luke 11:16 · Berean Standard Bible
And others tested Him by demanding a sign from heaven.
Context
14Basi Yesu alikuwa anamtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu aliyekuwa bubu. Yule pepo mchafu alipomtoka yule mtu aliyekuwa bubu, akaanza kuongea, nao umati wa watu ukashangaa. 15Lakini wengine wakasema, “Anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,* yule mkuu wa pepo wachafu wote.” 16Wengine ili kumjaribu wakataka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 17Yesu akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka. 18Kama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.