Native Bible

Leviticus 26:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae.

Leviticus 26:32 in English

Leviticus 26:32 · Berean Standard Bible

And I will lay waste the land, so that your enemies who dwell in it will be appalled.

Context

30Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana. 31Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu. 32Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae. 33Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa, na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu. 34Ndipo nchi itafurahia Sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Ndipo nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.