Walawi 19:21
Leviticus 19:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana.
Leviticus 19:21 in English
Leviticus 19:21 · Berean Standard Bible
The man, however, must bring a ram to the entrance to the Tent of Meeting as his guilt offering to the LORD.
Context
19“ ‘Mtazishika amri zangu.
“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.
“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.
“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti. 20“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru. 21Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana. 22Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake. 23“ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.