Walawi 18:28
Leviticus 18:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia.
Leviticus 18:28 in English
Leviticus 18:28 · Berean Standard Bible
So if you defile the land, it will vomit you out as it spewed out the nations before you.
Context
26Lakini ni lazima uzitunze amri zangu na sheria zangu. Mzawa na wageni waishio miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, 27kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi. 28Kama mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia. 29“ ‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao. 30Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.