Walawi 16:31
Leviticus 16:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu.
Leviticus 16:31 in English
Leviticus 16:31 · Berean Standard Bible
It is a Sabbath of complete rest for you, that you may humble yourselves; it is a permanent statute.
Context
29“Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge, wala msifanye kazi yoyote, iwe mzawa au mgeni anayeishi miongoni mwenu, 30kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha mtakuwa safi mbele za Bwana kutokana na dhambi zenu zote. 31Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu. 32Kuhani ambaye ametiwa mafuta na kuwekwa wakfu ili kuingia mahali pa baba yake kama kuhani mkuu atafanya upatanisho. Atavaa mavazi matakatifu ya kitani, 33na kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, na pia kwa ajili ya makuhani, pamoja na jumuiya yote ya watu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.