Walawi 13:18
Leviticus 13:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona,
Leviticus 13:18 in English
Leviticus 13:18 · Berean Standard Bible
When a boil appears on someone’s skin and it heals,
Context
16Hiyo nyama mbichi ikigeuka na kuwa nyeupe, ni lazima amwendee kuhani. 17Kuhani atamchunguza, na kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi. 18“Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona, 19napo mahali palipokuwa na jipu pakatokea uvimbe mweupe, au alama yenye wekundu na weupe, ni lazima akajionyeshe kwa kuhani. 20Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umezama ndani ya ngozi, na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.