Walawi 12:3
Leviticus 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mvulana atatahiriwa siku ya nane.
Leviticus 12:3 in English
Leviticus 12:3 · Berean Standard Bible
And on the eighth day the flesh of the boy’s foreskin is to be circumcised.
Context
1Bwana akamwambia Mose, 2“Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. 3Mvulana atatahiriwa siku ya nane. 4Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, mpaka siku za kutakaswa kwake zimetimia. 5Kama akimzaa mtoto wa kike, mwanamke huyo atakuwa najisi kwa majuma mawili, kama wakati wake wa hedhi. Kisha atasubiri kwa siku sitini na sita, ndipo atatakaswa kutoka damu kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.