Walawi 11:38
Leviticus 11:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu.
Leviticus 11:38 in English
Leviticus 11:38 · Berean Standard Bible
but if water has been put on the seed and a carcass falls on it, it is unclean for you.
Context
36Lakini chemchemi au kisima, mahali pa kuchota maji, patakuwa safi, lakini yeyote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi. 37Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zozote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi. 38Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu. 39“ ‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, yeyote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi mpaka jioni. 40Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.