Native Bible

Leviticus 1:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande.

Leviticus 1:6 in English

Leviticus 1:6 · Berean Standard Bible

Next, he is to skin the burnt offering and cut it into pieces.

Context

4Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 5Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Aroni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. 6Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande. 7Wana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. 8Kisha wana wa Aroni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.