Maombolezo 4:3
Lamentations 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.
Lamentations 4:3 in English
Lamentations 4:3 · Berean Standard Bible
Even jackals * offer their breasts to nurse their young, but the daughter of my people has become cruel, like an ostrich in the wilderness.
Context
1Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake,
dhahabu iliyo safi haingʼai!
Vito vya thamani vimetawanywa
kwenye mwanzo wa kila barabara. 2Wana wa Sayuni wenye thamani,
ambao mwanzo uzito wa thamani yao
ulikuwa wa dhahabu,
sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo,
kazi ya mikono ya mfinyanzi! 3Hata mbweha hutoa matiti yao
kunyonyesha watoto wao,
lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma
kama mbuni jangwani. 4Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga
umegandamana na kaakaa la kinywa chake,
watoto huomba mkate,
lakini hakuna yeyote awapaye. 5Wale waliokula vyakula vya kifahari
ni maskini barabarani.
Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau
sasa wanalalia majivu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.