Maombolezo 2:6
Lamentations 2:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. Bwana amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.
Lamentations 2:6 in English
Lamentations 2:6 · Berean Standard Bible
He has laid waste His tabernacle like a garden booth; He has destroyed His place of meeting. The LORD has made Zion forget her appointed feasts and Sabbaths. In His fierce anger He has despised both king and priest.
Context
4Ameupinda upinde wake kama adui,
mkono wake wa kuume uko tayari.
Kama vile adui amewachinja
wote waliokuwa wanapendeza jicho,
amemwaga ghadhabu yake kama moto
juu ya hema la Binti Sayuni. 5Bwana ni kama adui;
amemmeza Israeli.
Amemeza majumba yake yote ya kifalme
na kuangamiza ngome zake.
Ameongeza huzuni na maombolezo
kwa ajili ya Binti Yuda. 6Ameharibu maskani yake kama bustani,
ameharibu mahali pake pa mkutano.
Bwana amemfanya Sayuni kusahau
sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake;
katika hasira yake kali amewadharau
mfalme na kuhani. 7Bwana amekataa madhabahu yake
na kuacha mahali patakatifu pake.
Amemkabidhi adui kuta
za majumba yake ya kifalme;
wamepiga kelele katika nyumba ya Bwana
kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa. 8Bwana alikusudia kuangusha
ukuta uliomzunguka Binti Sayuni.
Ameinyoosha kamba ya kupimia
na hakuuzuia mkono wake usiangamize.
Alifanya maboma na kuta ziomboleze,
vyote vikaharibika pamoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.