Maombolezo 2:3
Lamentations 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika hasira kali amevunja kila pembe* ya Israeli. Ameuondoa mkono wake wa kuume alipokaribia adui. Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka.
Lamentations 2:3 in English
Lamentations 2:3 · Berean Standard Bible
In fierce anger He has cut off every horn * of Israel and withdrawn His right hand at the approach of the enemy. He has burned in Jacob like a flaming fire that consumes everything around it.
Context
1Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni
kwa wingu la hasira yake!
Ameitupa chini fahari ya Israeli
kutoka mbinguni mpaka duniani,
hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu
katika siku ya hasira yake. 2Bila huruma Bwana ameyameza
makao yote ya Yakobo;
katika ghadhabu yake amebomoa
ngome za Binti Yuda.
Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake
chini kwa aibu. 3Katika hasira kali amevunja
kila pembe* ya Israeli.
Ameuondoa mkono wake wa kuume
alipokaribia adui.
Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao
ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka. 4Ameupinda upinde wake kama adui,
mkono wake wa kuume uko tayari.
Kama vile adui amewachinja
wote waliokuwa wanapendeza jicho,
amemwaga ghadhabu yake kama moto
juu ya hema la Binti Sayuni. 5Bwana ni kama adui;
amemmeza Israeli.
Amemeza majumba yake yote ya kifalme
na kuangamiza ngome zake.
Ameongeza huzuni na maombolezo
kwa ajili ya Binti Yuda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.