Maombolezo 2:18
Lamentations 2:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mioyo ya watu inamlilia Bwana. Ee ukuta wa Binti Sayuni, machozi yako na yatiririke kama mto usiku na mchana; usijipe nafuu, macho yako yasipumzike.
Lamentations 2:18 in English
Lamentations 2:18 · Berean Standard Bible
The hearts of the people cry out to the Lord.* O wall of the Daughter of Zion, let your tears run down like a river day and night. Give yourself no relief, and your eyes no rest.
Context
16Adui zako wote wanapanua
vinywa vyao dhidi yako,
wanadhihaki na kusaga meno yao
na kusema, “Tumemmeza.
Hii ndiyo siku tuliyoingojea,
tumeishi na kuiona.” 17Bwana amefanya lile alilolipanga;
ametimiza neno lake
aliloliamuru siku za kale.
Amekuangusha bila huruma,
amewaacha adui wakusimange,
ametukuza pembe ya adui yako. 18Mioyo ya watu
inamlilia Bwana.
Ee ukuta wa Binti Sayuni,
machozi yako na yatiririke kama mto
usiku na mchana;
usijipe nafuu,
macho yako yasipumzike. 19Inuka, lia usiku,
zamu za usiku zianzapo;
mimina moyo wako kama maji
mbele za Bwana.
Mwinulie yeye mikono yako
kwa ajili ya maisha ya watoto wako,
ambao wanazimia kwa njaa
kwenye kila mwanzo wa barabara. 20“Tazama, Ee Bwana, ufikirie:
Ni nani ambaye umepata
kumtendea namna hii?
Je, wanawake wakule wazao wao,
watoto waliowalea?
Je, kuhani na nabii auawe
mahali patakatifu pa Bwana?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.