Maombolezo 2:14
Lamentations 2:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Maono ya manabii wako yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, hawakuifunua dhambi yako ili kukuzuilia kwenda utumwani. Maneno waliyokupa yalikuwa ya uongo na ya kupotosha.
Lamentations 2:14 in English
Lamentations 2:14 · Berean Standard Bible
The visions of your prophets were empty and deceptive; they did not expose your guilt to ward off your captivity. The burdens they envisioned for you were empty and misleading.
Context
12Wanawaambia mama zao,
“Wapi mkate na divai?”
wazimiapo kama watu waliojeruhiwa
katika barabara za mji,
maisha yao yadhoofikavyo
mikononi mwa mama zao. 13Ninaweza kusema nini kwa ajili yako?
Nikulinganishe na nini,
ee Binti Yerusalemu?
Nitakufananisha na nini,
ili nipate kukufariji,
ee Bikira Binti Sayuni?
Jeraha lako lina kina kama bahari.
Ni nani awezaye kukuponya? 14Maono ya manabii wako
yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu,
hawakuifunua dhambi yako
ili kukuzuilia kwenda utumwani.
Maneno waliyokupa
yalikuwa ya uongo na ya kupotosha. 15Wote wapitiao njia yako
wanakupigia makofi,
wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyao
kwa Binti Yerusalemu:
“Huu ndio ule mji ulioitwa
mkamilifu wa uzuri,
furaha ya dunia yote?” 16Adui zako wote wanapanua
vinywa vyao dhidi yako,
wanadhihaki na kusaga meno yao
na kusema, “Tumemmeza.
Hii ndiyo siku tuliyoingojea,
tumeishi na kuiona.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.